Mhe.Omar S. Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar ambaye ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 12 wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) wa Mawaziri unaoendelea mjini Geneva, Switzerland, akichangia mada inayohusu Changamoto za Ushirikiano wa Biashara ya Kimataifa WTO siku ya Ufunguzi wa Mkutano huo tarehe 12 Juni 2022.

Mhe. Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar na Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), unaoendelea mjini Geneva tangu tarehe 12-15Juni 2022, amewasilisha msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kuunga mkono maamuzi ya kuondoa Uzuiaji wa Chakula Kutoka Nje ya Nchi kinachonunuliwa na WFP kwa sababu za kibinadamu. Awali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilichelea kuunga mkono pendekezo hilo mpaka ilipojihakikishia kuwa uamuzi huo hautazuia nchi kuchukua hatau ya kuzuia ikiwa kuna tishio la usalama wa chakula.