Katika picha ni Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, akiwa amekutana na Bw. Fernandez-Taranco, Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeratibu suala la ushirikiano wa Maendeleo tarehe 14 Desemba 2022. 

Bw. Fernandez-Taranco, aliomba kukutana na Balozi Tarishi, ambaye ni Mwenyekiti wa Wawakilishi wa nchi za Kundi la 77 na China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva tangu Oktoba 2022 hadi Desemba 2023, kumpatia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi yake katika kuratibu ushirikiano wa maendeleo.