Leo tarehe 15 Julai 2022, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria akiwa ameambatana na Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi na Mhe. Hoyce Temu, Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva amefanya mazungumzo na Bi. Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya Ngorongoro.
Kwa upande wake, Bi. Bachelet ameshukuru na kupongeza kwa namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza masuala ya haki za binadamu hususan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.