Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Dkt. Grace Magembe, Naibu Katibu Mkuu, OR TAMISEMI washiriki kikao kazi cha Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) kilichoanza tarehe 28 Novemba, 2022 Geneva, Uswisi.
Lengo la kikao ni pamoja na kujadili hatua zilizofikiwa katika kutekeleza miradi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji Mifumo ya Afya (2021- 2023). Vilevile, kujiandaa kwa andiko jipya litakalotekelezwa (2024 -2026) ambalo litalenga kutokomeza magonjwa hayo matatu kabla ya mwaka 2030 pamoja na kuimarisha mifumo ya afya na ubora wa huduma za afya.
Prof. Makubi alishukuru ofisi ya Ubalozi Tanzania Geneva kwa kusimamia vema masuala ya sekta ya afya nchini Uswisi ambapo ndipo kuna mashirika mengi ya kimataifa yanayoshughulikia masuala ya afya.
