1. Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu, ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanyiwa tathmini ya Haki za Binadamu. 2. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (Mb.) ameongoza Ujumbe wa Tanzania ambapo ameeleza hatua mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye masuala mbalimbali ya Haki za Binadamu nchini Tanzania ikiwemo Elimu, Afya, Haki za Watoto, Wanawake, wenye ulemavu, Haki za Kisiasa na mengine mengi. 3. Tathmini ya Tanzania imekubaliwa na Baraza hilo, nchi 23 zilizoizungumzia Tanzania kwa hatua nzuri zilizofanyika katika kuhakikisha Haki za Binadamu zinazingatiwa. Pia wamekumbusha Tanzania kuendelea kutatua changamoto zilizobaki.