Mkutano Mkuu wa mwaka wa WIPO umefunguliwa leo tarehe 14 Julai 2022, Geneva Uswisi. Katika picha ni Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Maimuna K. Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Wengine walioshiriki (wa kwanza kulia kwa Mhe. Balozi) ni Bw. Mr. Godfrey Simango Nyaisa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA), na (wa kwanza kushoto kwa Mhe. Balozi) ni Bi. Mariam Mliwa Jecha, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Biashara na Leseni Zanzibar na anayefuatia ni Bi. Magdalena Utouh, Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa bidhaa hafifu, kutoka Tume ya Ushindani Tanzania (FCC). Wa mwisho (kulia kwa Mhe Balozi) ni  Bi. Loy Mhando Msajili Mkuu msaidizi, Kutoka Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA).