Tarehe 29 Juni 2022, Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, Geneva alimpongeza Bi. Michelle Bachelet kufuatia kumaliza kwa muda wake katika nafasi aliyokuwa akihudumu ya Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.  Pia, Mhe. Balozi alimhakikishia Bi. Bachellet kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza ushirikiano na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Aidha, Mhe. Balozi alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na hifadhi ya Ngorongoro, na kuhimiza Jumuiya ya Kimataifa kuepuka kuamini taarifa za upotoshwaji zinazoenezwa kuhusu maeneo hayo; na kuwa hakuna mkazi yoyote aneyeondolewa kwa nguvu kama inavyodaiwa.

Alihitimisha kwa kueleza kwamba Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wake.