Mhe. Maimuna Tarishi,  Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, Geneva, tarehe 21 Julai 2022 amekutana na kuwa na mazungumzo na Mhe. Jérôme Bonnafont, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Geneva, aliefika katika Ofisi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mazungumzo yao yalijikita zaidi katika masuala ya kuendelea kupigania haki za wanawake na watoto wakike, na teknolojia ya habari na Mawasiliano. Wamekubaliana kuiamarisha na kuendeleza ushurikiano katika maeneo hayo, na katika shughuli za Baraza la Haki na Binadamu la Umoja wa Mataifa.