Leo tarehe 12 Aprili 2022, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu Geneva, Mhe. Maimuna Tarishi amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Victor Mutasi (kulia kwa Mhe. Balozi), Mtanzania ambaye yupo Geneva kushiriki Mkutano wa Vyuo Vikuu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu Biashara za Kimataifa katika Shirika la Biashara Duniani(WTO). Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bw. George Ngolwe, Afisa Biashara kutoka  Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambaye yuko Geneva akihudhuria mafunzo kwa vitendo, WTO.